
KIONGOZI/A LEADER: Kabla ya yote kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa yote anayoendelea kutujaria ktk maisha yetu. Leo nimependa kuwashirikisha kuhusu kiongozi ni nani? Na sifa bora za kiongozi. Kwani kwa namna yoyote ile sisi sote ni viongozi kwani uongozi haukwepeki popote utakapokwenda itafikia kipindi itakulazimu uwe kiongozi. Kama sio wa serikali basi dini na kama sio hapo basi familia. Sasa basi kwa namna yoyote ile kujifunza kuhusu uongozi au kiongozi bora hakuepukiki. Ndugu zangu uongozi unabeba vitu vingi sana ktk maisha yetu kwani ukihitaji kuwa na mafanikio ya aina yoyote ile yanahitaji kupitia kwenye misingi ya uongozi bora. Kwa mfano: ukitaka maendeleo ya kiuchumi lazima uongozi bora utahitajika, ukitaka familia bora lazima uongozi bora utahitajika, ukitaka Amani ktk nchi lazima uongozi bora unahitajika. Yaani ni mahali popote uongozi bora uhahitajika. Kwa ufupi sana leo tutakwenda kujifunza na ...