KIONGOZI/A LEADER:



Kabla ya yote kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa yote anayoendelea kutujaria ktk maisha yetu. Leo nimependa kuwashirikisha kuhusu kiongozi ni nani? Na sifa bora za kiongozi. Kwani kwa namna yoyote ile sisi sote ni viongozi kwani uongozi haukwepeki popote utakapokwenda itafikia kipindi itakulazimu uwe kiongozi. Kama sio wa serikali basi dini na kama sio hapo basi familia. Sasa basi kwa namna yoyote ile kujifunza kuhusu uongozi au kiongozi bora hakuepukiki. Ndugu zangu uongozi unabeba vitu vingi sana ktk maisha yetu kwani ukihitaji kuwa na mafanikio ya aina yoyote ile yanahitaji kupitia kwenye misingi ya uongozi bora. Kwa mfano: ukitaka maendeleo ya kiuchumi lazima uongozi bora utahitajika, ukitaka familia bora lazima uongozi bora utahitajika, ukitaka Amani ktk nchi lazima uongozi bora unahitajika.  Yaani ni mahali popote uongozi bora uhahitajika. Kwa ufupi sana leo tutakwenda kujifunza na kushirikishana kuhusu kiongozi ni nani? Na sifa za kiongozi bora.

KIONGOZI ni yule anayesimamia anachokiamini!,anasimamia maamzi yake.

Tukizingatia maana hiyo moja kwa kifupi. Hebu tuangalie neno lenyewe KIONGOZI:
K - kubari kushauriwa
I - Ielewe hali ya mahali ulipo.
O – Onesha mifano kwa vitendo.
N – Nena kauri thabiti na zenye kutekerezeka.
G – Gawa majukumu.
O – Ondoa upendereo.
Z – Zuia mipasuko yoyote ile ndani na nje ya taasisi au kampuni.
I – Inua kiwango cha utendaji wa kazi.

Aliwahi kusema John Quincy Adams
“Kama matendo yako yanawahamasisha wengine kupata ndoto zaidi, kujifunza zaidi, kufanya na kuwa zaidi, wewe ni kiongozi.”

Kumbe Kiongozi anajulikana kwa matendo yake.

Katika makala hii utaweza kufahamu sifa 10 zitakazokufanya kuwa kiongozi bora.

1. Uwazi na ukweli.

Uwazi na ukweli ni sifa muhimu inayomfanya mtu kuwa kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima awe wazi katika utendaji kazi wake pia awe mkweli siku zote.Uwapo kiongozi kuna siri za kazi lakini namna ya utendaji kazi hautakiwi uwe siri au usioeleweka kwa wale unaowaongoza. Kiongozi bora anatakiwa kuwa na mpangilio mzuri na unaoeleweka wa utendaji kazi wake.(isaya 56:1) zingatieni mema na kutenda haki.

2. Maono.

Aliwahi kusema John C. Maxwell
“Kiongozi ni yule anayejua njia, anakwenda njia hiyo na anaonyesha njia.”

Maono ni picha inayojengeka katika fikira ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa.Kama wewe ni kiongozi usiyeweza kuona picha ya baadaye ya kampuni au taasisi hutaweza kuiongoza kampuni kufikia mafaniko na malengo yake. Jitahidi kujifunza kuwa na maono katika jambo lolote unalolifanya ili lifanikiwe.

3. Uadilifu.

Ili uwe kiongozi bora huna budi kuwa mwadilifu. Heshimu kazi, tunza muda, tunza fedha pia tumia nafasi yako kwa njia ambayo si ya kibadhirifu.Ni rahisi mtu kushawishika kutumia ofisi au nafasi ya kiuongozi kwa maslahi binafsi jambo ambalo linamfanya kupoteza sifa yake ya kiongozo bora. Kiongozi lazima awe na fadhila za uadilifu( busara,haki,nguvu na kiasi).

4. Ujasiri.

Huwezi kuwa kiongozi bora kama hutakuwa na ujasiri katika maswala mbalimbali. Unahitaji ujasiri kufanya maamuzi mbalimbali katika eneo au taasisi unayoiongoza kama vile kufanya uwekezaji mpya, kubadili mfumo wa utendaji kampuni au taasisi n.k.Lazima kiongozi aoneshe ujasiri kwa watawaliwa au wafanyakazi wengine katika maamuzi yake anayoyafanya kila siku.

5. Subira/ uvumilivu.

Kuna mambo yanayohitaji subira katika maisha. Kiongozi asiye bora hutaka kila kitu kitimie kwa siku moja. Kuwa kiongozi mkomavu ni kuwa na subira na uvumilivu.Wakati mweingine kampuni au taasisi yako inaweza kuwa inapita kwenye kipindi kigumu; usipokuwa kiongozi mwenye subira unaweza kufanya maamuzi ambayo yataathiri kampuni au taasisi daima.

6. Mbunifu.

Aliwahi kusema  Steve Jobs
“Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”

Kufanikiwa kwa kampuni au taasisi kunahitaji ubunifu wa hali ya juu kila mara. Hivyo basi ili uweze kuwa kiongozi bora jitahidi kuwa mbunifu.Buni mbinu, mawazo na miradi mbalimbali ambayo itawezesha kampuni au taasisi kukua na kufikia malengo yake.Epuka kutegemea mawazo ya zamani hata kama bado yanailetea kampuni faida kwani mambo yanaweza kubadilika wakati wowote.

7. Uwajibikaji na Kujituma

Aliwahi kusema  Allen West
“Uongozi ni kuwa mtumishi kwanza.”

Ukitaka kuwa kiongozi bora huwezi kujitenga na uwajibikaji. Lazima uwajibike kutimiza majukumu yako yote.Utawezaje kuwaongoza na kuwahimiza wengine kutimiza majukumu yao kama wewe mwenyewe huwezi kutimiza majukumu yako? Nasisitiza tena kwa kusema wajibika katika nafasi yako na wale unaowaongoza watawajibika katika nafasi zao.Kujituma ni jambo muhimu sana kwa kiongozi bora. Kiongozi bora hahitaji sheria na usimamizi mkali ili atimize majukumu yake. Hivyo basi, ukitaka kuwa kiongozi bora ni lazima ujifunze kujituma bila kusukumwa na mtu. Fanya bidii uwapo kazini au katika nafasi yako yaa kiuongozi; hili litakujenga na kukufanya kuwa kiongozi bora.

8. Mawasiliano/lugha.

Mawasiliano ni swala muhimu sana linalojenga utawala bora. Katika taasisi au kampuni isiyokuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano lazima kutatokea migongano na misuguano isiyokuwa na sababu.Ukiwa kiongozi hakikisha unakuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano na watu wengine katika taasisi au kampuni unayoiongoza. Hakikisha pia unajenga mfano mzuri wa kutoa taarifa katika kampuni au taasisi iliyopo.

9. Nidhamu na maadili.

Kuna mambo ambayo huwezi kufanya unapokuwa kiongozi hata kama wengine wanayafanya au unavutiwa nayo. Siku zote epuka tabia zisizo endana na kiongozi bora kama vile ulevi, umbeya, uvivu, anasa, strarehe kuongea hovyo n.k. Onesha watu unaowaongoza kuwa wewe ni kiongozi mwenye uelewa uliokujengea nidhamu na kujitawala. Kiongozi akemee maovu bila woga bila haya (2 tim 4:3   3:15-16).

10. HOFU YA MUNGU.

Kiongozi yoyote mzuri ni lazima awe na hofu ya Mungu. Kwani kupitia misingi hiyo mizuri ya kimungu atajari mahitaji muhimu ya watu anaowaongoza, Atajari utu wa mtu, kupitia sala atakuwa na ulinzi wa kutosha, pia atatimiza wajibu wake ipasavyo. Kiongozi lazima awe na fadhila za kimungu(Imani,matumaini na mapendo).

Hitimisho

Hakika kwa kutumia sifa hizo 10 amabazo nimekueleza kukuwezesha kuwa kiongozi bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko katika taasisi au kampuni unayoiongoza kama hutojifuza kuwa kiongozi bora.wewe kiongozi sasa unatumwa nenda kawe chumvi na mwanga kwa wenzako.

ZINGATIA HAYA KTK UTUME/UONGOZI WAKO.


  • Ondoa hofu, jaa ujasiri (isaya 41:10).
  • Kalipia ,kemea, onya (2 tim 4:2).
  • Vaeni silaha zote za Mungu(efso 6:10-18).
  • Mtafuteni Mungu siku za maisha yenu yote.(Efes 5:1-6), nanyi mtanitafuta na kuniona matakaponitafuta kwa moyo wenu wote (yeremia 29:13), wala yeyote ajaye kwangu sitomtupa nje kamwe. (yohana 6:37).
  • Kesheni, jilindeni mkiomba( sala ndio ant-virus ya viongozi).
  • Furahini daima ktk kutimiza utume wenu, jitoeni sadaka.(filp 2:17-18).
  • Ninyi ni chumvi ya dunia , ninyi ni mwanga wa ulimwengu( mt 5: 13-16).
  • Mzidi kuwa hodari ktk bwana(efeso 6:10).
  • Ishikeni amri iliyokuu ya upendo/mapendo kwani ni hatari sana mtu mwenye mamlaka au maarifa kuwa hana upendo kwa wengini. 
WELCOME TO MY BLOG.  LET US WALK TOGETHER. 

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU JINSI YA KUFANYA BIASHARA KIPINDI CHA MAGUFULI

CHALLENGE IS PART OF HUMAN LIFE