FAHAMU JINSI YA KUFANYA BIASHARA KIPINDI CHA MAGUFULI
Sababu zinazowafanya watu kufunga
frem kila kona ni nini??
Ninashindwa kuelewa
kipindi hiki imekuwaje?? kuna nini?? kulikoni?? mbona kila
pande za nchi ukipita maduka na frem nyingi zimefungwa?? eti watu wanadai
maisha ni magumu. swali la kujiuliza je ukifunga frem ndo suruhisho sahihi la
kuyafanya maisha yawe rahisi?? kama wewe ni mfugaji unahisi kuuza mifugo na
kuchinja yote ni suruhisho sahihi?? na kama wewe ni mkulima unahisi kufungia jembe
ndani ndio suruhisho la kufanya maisha kwako yasonge???
Hii inatokea kwa sababu
watu wengi tulikuwa tumezoea kufungua biashara zetu kwa mazoea bila kujua mambo
mhimu yanayotakiwa ktk biashara ni yapi?? Mtu anafuga lakin hajuwi anatumia
njia gani ya kufuga au mtu analima hajui kesho mvua isiponyesha atafanyeje ili
mazao yake yasiwe na shida.
wengi wetu tulikuwa
tunafanya shughuri zetu za kibiashara kwa mazoea na bila tahadhari yoyote. bila
ya kujua kwamba ktk biashara yoyote ile tahadhari ni kitu kikubwa sana. umewahi
kujiuliza kwanini wataaramu wanatushauri tuwa na bima za biashara na afya zetu.
hii ni kwa sababu ya tahadhari kwa chochote kitakacho tokea.
leo napenda kukujuza vitu vichache tu katika
biashara:
naomba tuwe pamoja kwa haya. kwani katika biashara
unatakiwa kujua mambo yafuatayo;
1. Lengo la
biashar: kwanini umeamua kufanya
biashara hiyo?? kila mtu anayeanzisha biashara anatakiwa kuwa na lengo maalumu
na biashara yake. kwani unapoanzisha biashara bila ya lengo maalum itakusumbua
kujua unaelekea wapi katika biashara yako. wapo watu anafanya biashara ili
mladi ck zisongee mbele. huyu mtu hana malengo yoyote na biashara hiyo just
anafanya tu kwa mazoea. au kwa vile mama, shangazi au baba alikuwa anafanya
kazi hiyo.[tubadilike].
2. Mipango ya biashara{business plan}: Lazima kabla ya hata kuanzisha biashara yako. upate
mpango kazi wa biashara yako.{business pla}. hapa ndo uwanja wangu sasa wa
kujidai. kwani watu wengi wamekuwa na tabia ya kufanya biashara bila mipango.
namaanisha yakuwa kufanya biashara bila mipango ni sawa na kuuziwa mbuzi kwenye
gunia. unfanya kitu ambacho hukijui au hukifahamu. hatari sana hii.
naomba twende pamoja:
ndani ya business plan kuna vitu vya msingi unatakiwa kuvijua.kwa ufupi wake;[tubadirike].
(a) Masoko(market): kabla hata hujaanzisha biashara yako unatakiwa
kujua soko lako ni lipi?? ndani ya kipengere cha masoko kuna vitu vya
kuangalia kama vile wateja wako ni kina
nani?(your customers). sehemu unapotaka
kuanzishia biashara yako(location), matangazo(promotion/advisement ), bei (price)
N.k viko vingin sana. kabla hujaanzisha biashara yako unatakiwa kuvijua vyote
hivyo ili vikupe maamuzi yaliyo sahihi.[tubadirike].
(b). Usimamizi(management): watu wengi sana tumekuwa tukilia kuhusu biashara zetu. kwani ni ukweli usiofichika yakuwa
biashara ni usimamizi. sasa basi unapoanzisha biashara yoyote ili lazima ujue
utawezaje kuisimamia?? ndipo utagundua kuna umhimu wa kuwa na management plan
kabla ya biashara yako kuanza.hapa napo kuna mambo mengi sana ya kuangalia kwa
leo siwezi kuyaelezea yote.[tubadirike].
(c). Uzalishaji(production): kama wewe biashara yako ni ya uzalishaji. kabla ya
kufungua biashara yako unatakiwa kujua uzalishaji unaoenda kuufanya utakuwaje
na kwa namna gani?? hata kama ni mandazi hiyo ni aina ya uzalishaji. lakini cha
kushangaza tumekuwa tukifanya biashara zetu kwa mazoea.[tubadirike].
(d). kifedha(financial plan): lazima ujue mtaji ulionao na uweke mipango
kulingana na mtaji wako. hapo utajua ni namna gani utaendesha mambo yako kwa
mtaji ulionao. sio mtu unaanza biashara tu hujui hata garama za uendeshaji wa
hiyo biashara yako.[tubadirike].
(e) Uendeshaji( operation): unatakiwa kujua garama za uendeshaji wa biashara
yako kabla hata hujaanza biashara yako.yaani ukipiga picha kabla ya yote unatakiwa kuona kila kitu mbele kuna nini???. kwa mfano; kuna watu kisa tu anapesa za
kununua mashine fulani baisi hajui hata huduma za mashine hiyo yaani maintenance.
unakuta matu huyo ananunua mashine ambayo garama za kuihudumia ni zaidi ya
kuinunulia. je huyo mtu kwa wakati kama huu atakuwa salama??? zaidi ya kufunga
frem???[tubadirike].
3. Ubunifu (creativity): katika biashara lazima kuwe na ubunifu ili kuendana
na mazingira na mabadiriko ya hali ya kiuchumi. usipokuwa mbunifu wewe katika
maisha yako utakuwa msindikizaji tu na mtu wa kwanza kufunga frem. sio kwamba
wote waliofunga frem hawana ubunif. no. ila ubunifu ni kitu mhimu sana katika
biashara.[tubadirike].
1. Tubadirike kutoka
kwenya hali ya mazoea na kuja kwenye hali ya uhalisia. usifanye kitu ili mladi
tu unakifanya. inatakiwa kweli unadhamilia na kukiwekea mipango na malengo. kama ni biashara unatakiwa kuweka mipango madhubuti ya kutangaza biashara yako na uendeshaji[tubadirike].
2. Tufanye biashara kwa
tija, tufuge kwa tija na tulime kwa tija: namaanisha tufuate taratibu za
ufanyaji wa biashara na taratibu za ufugaji wa tija pia kulima kwa tija.[tubadirike].
3.wananchi tunatakiwa
kuyafahamu haya na kuyajua kwa undani. kwani katika halimashauri zetu tunao
wataaramu wetu. tuwatumie hao ili kutuelimisha yote haya. mabwana mifugo wapo,
mabwana shamba wapo, maafisa biashara wapo. je kama wananchi hatuyafahamu haya wao
wanafanya kazi gani huko maoffisi kwao??? kwani ni wajibu wao kutuelimisha sisi
wananchi. au wao tunavyofunga frem zetu na kuchinja mifugo yetu wao
wanafurahi?? tuwatumie hao ili tuweze kufuga kwa tija, kulima kwa tija na
kufanya biashara kwa tija.[tubadirike].
mbali na hapo unaweza ukawasiliana
na sisi kwa msadaa zaidi. ukatueleza unataka kufanya kilimo, ufugaji au
biashara gani ili kukusaidia mawazo na mipango ni wapi pa kuanzia au wapi pa kuboresha
kama una biashara yako tayari. tutakushauli kulingana na eneo ulipo na hali
uliyonayo; kwani kwa uzoefu tumesaidia wengi.[tubadirike].
nawatakieni heri na baraka katika shughuri zenu za
kila siku.
welcome to my blog. let us walk together.
Comments
Welcome to my blog. Let us walk together.