SIRI YA KUWEZA KUFIKIA NDOTO YAKO
Katika maisha UKIANGUKA NYANYUKA KISHA ENDELEA NA SAFARI YAKO HUKO UENDAKO: Kwani hiyo ndiyo siri kubwa ambayo wengi wetu tunashindwa kufikia malengo yetu baada ya kuanguka kupitia changamoto za hapa na pale. tunashidwa kujua tumeangukia wapi?? na ukishajua ulipoangukia inapendeza na inafurahisha kukupa wewe uzoefu wa kutoanguka tena au uwezo wa kubadiri njia ya kupita ili safari yako ufike huko uendako.
Tazama mfano huu. nataka ujifunze kitu.
Katika maisha kawaida mtoto anapoanza kutembea, huanguka mara kadhaa, lakini hakati tamaa huendelea na mazoezi ya kujifunza kutembea na mwisho huweza kutembea mwenyewe. Mara nying watu wazima humcheka wakisahau kwamba hata wao walianza kama yeye!! pamoja na hayo mtoto haoni fedhea, huendelea na mwisho hufanikiwa. Hivyo ndivyo binadamu yeyote anapaswa kuwa katika maisha kwa lengo la kujiletea mabadiliko Fulani yawe ni ya binafsi au jamii; Fedheha na kukata tama si mambo ya kuendekeza hata kidogo. kwa kawaida binadamu hujiona mnyonge anapofanya jambo Fulani na kushindwa!!! Biashara, masomo au mipango mingine yeyote ya kimaisha.
Katika maisha yafaa tutambue kuwa ili kuwa washindi ni lazima kuna kupitia milima na mabonde. hii ni pamoja na kuanguka ktk changamoto. yatupasa kujua hili kwamba kushindwa, kuchekwa, kudhalauliwa na kukejeliwa ndipo ushindi wetu tunakoupata.
Katika maisha yote haya wewe usiogope kuwa jasiri kama mtoto. jiamini ktk yote unayoyafanya yote utafanikiwa.
TAKE YOUR DREAM, HOLD YOUR DREAM, WALK WITH YOUR DREAM AND LIVE YOUR DREAM. LAST ENJOY YOUR DREAM.
welcome to my blog. let us walk together.
Comments