TOKOMEZA UJINGA TUJENGE UCHUMI WA NCHI YETU

 *SOMA MPAKA MWISHO*


Kwa majina naitwa *Eng. SAIMON MATHEW NDAKI*. Ni mhitimu wa chuo kikuu cha kilimo SUA (SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE) 2015/2019. Nimesomea fani ya uhandisi katika sector ya viwanda.  Bcs:  In Bioprocess and Post harvest Engineering. kwa kiswahili. mhandisi wa uchakataji, usindikaji na uhifazi wa mazao ya kilimo. *Binafsi mimi ni mdau na mkeleketwa wa sector ya elimu hapa nchini* Ni katika harakati za kupambana na adui ujinga anayetafuna Taifa letu. 

Pamoja na utambulisho huo mfupi.  Awali ya yote Nipenda kuchukua nafasi hii kukuomba ushilikiano wako wa dhati kwani natambua juhudi,  jitihada na mchango wako katika sector ya elimu hapa nchini. Ninachokiamini Mimi bila elimu bora nchi yetu haiwezi kuendelea kupiga hatua bila ya kuwa na wasomi wazuri Kwa fani tofauti tofauti kwani elimu ni pamoja na technolojia na technolojia ni maarifa.  Kwa kulitambua hilo kama mzalendo wa kweli na nchi yangu nimeamua kuwekeza nguvu, akili na utashi wangu wote katika kuhakikisha sector ya elimu inasonga mbele na kufanya mageuzi makubwa katika sector hii. Ikiwa kwa mawazo, ushauri na sapoti ya aina yoyote ile pale panapo wezekana.

Nimeamua kufanya hivyo baada ya kuona uhitaji wa nchi yangu. lakini mimi Kama kijana

Baada ya serikali kutuletea mfumo na mpango ya elimu bure ni dhahiri na ukweli kabisa yakuwa watoto wetu wanakwenda shule kwa wingi na mwitikio tumeuona. Kilichobaki ni kuhakikisha tunajaribu kuwaza na kuwazua ni kwa namana gani watoto wetu watafanya vizuri katika masomo yao? *Hili sio swala la kuitupilia serikali pekee yake bali ni swali ambalo kila mtanzania anatakiwa ajiulize na kulitafutia ufumbuzi*  kwani *"mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe*”  kwa pamoja tutajenga nchi yetu.

Baada ya kukaa chini na kuliwaza hilo nimeamua kuja na wazo la kufanya program ya uhamasishaji nchi nzima kuliona hili kwa mapana yake na kuchukua hatua stahiki kwa wazazi na watoto kwa ujumla wake. Program yangu itakwenda kwa “TOKOMEZA UJINGA, TUJENGE UCHUMI WA NCHI YETU”.

Program yangu itajikita zaidi kutowa hamasa kwa watoto wanaofanya vizur katika masomo yao kuanzia ngazi ya darasa la kwanza hadi la saba. Ninasimama mbele ya watanzania wote kuwaomba kila mmoja wetu aliyewahi kupitia elimu ya shule ya msingi popote pale nchini aniunge mkono kwa kuhakikisha analudi shule ile ile aliyopitia yeye na kumtoa ujinga kwa kutoa sapoti ya kuwawezesha vijana wetu wanaofanya vizuri angarau hata kwa kuwapatia kalamu tu kila anayekuwa wa kwanza darasani anapata kalamu bure mwaka mzima. kwa hamasa hiyo mimi ninaamini kabisa ni kitu kidogo sana ila kama watanzania wote tukiungana na kukifanya kwa uzalendo wetu. Ninayo imani kubwa sana katika hili, yakwamba litaleta mabadiliko makubwa sana ndani ya nchi yetu na kufanya watoto wetu wahamasike na kuona fursa ya kushindana kwa hamasa kubwa darasani. Box moja la kalamu ya wino 50 ni Tsh 5,000/=  tu kiwango ambacho kila mtanzania anayethamini elimu anao uwezo wa kuchangia. Hii pia ni kama shukrani kwa Mungu kuweza kurudisha sapoti(mchango) yako kwa shule uliyosomea. Amini, amini, nakwambia, siwahukumu ila ninawakumbusha tu yakwamba wapo watu wasomi ngazi mbalimbali Prof, Dr, Eng, Mwl n.k lakini tangu amalize shule ya msingi hajawahi tena kufika shule aliyosoma hata kwenda kusalimia tu. Sasa nimeamua mwaka 2021 tufanye kuwa mwaka wa historia kwa kila mmoja wetu kurudi na kwenda kusalimu alikotoka. Kwa uzalendo, nia na kuwajibika sote tutaijenga nchi yetu.


*FAIDA ZA PROGRAM/MPANGO HUU*.

1. Kufanikiwa kwa zoezi hili kutaleta mapinduzi makubwa katika nyanja ya elimu kwani wapo wadau mbalimbali wa elimu hawatoishia kutoa kalamu tu ila watatizama na changamoto zingine ambazo zinaikabili shule husika kama vile ukosefu wa miundo mbinu ya madawati, madarasa na vitendea kazi vingine.

2. Kutajenga utayali, umakini na ushilikiano mkubwa kati ya jamii na serikali kwenye suala zima la elimu haswa katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sector ya elimu nchini.

3. Kukua kwa sector ya elimu nchini kwani mimi ninayo imani yakuwa suala hili litaongeza ushindani darasani na kufanya watoto wetu wasome kwa bidii zote nahii kuongeza ufauru wa wanafunzi kwani suala hili linamgusa mtoto moja kwa moja.

4. Kujenga na kukuza uzalendo wa nchi na wananchi wake.

5. Tutaisaidia wizara ya elimu kupata taarifa pia kuibua changamoto mbalimbali zinazopelekea kuwa kikwazo cha kusonga mbele na kutafuta ufumbuzi.

Pamoja na hayo yote italeta chachu kwa watoto wenyewe na kuwafanya watamani kutimiza Ndoto walizo nazo yaaani (inspiration program and self determination).kwa kuona watu walio fanikiwa kupitia shule yao kumbe wapo pamoja nao.


Hizo ni baadhi tu ya faida ambazo nimeweza kuzitaja hapa ila ziko nyingi Sana.


BINAFSI NIMEANZISHA PROGRAM AMBAYO KUPITIA WEWE LEO NINAOMBA SUPORT YENU YA HALI NA MALI KUHAKIKISHA NINATIMIZA AZIMA YANGU YA KUWA SEHEMU YA WATU WANAOPINGANA NA UJINGA KTK NCHI YETU. 


My program dealing with insperation and motivation program for primary student.


*Njinsi ya kuniunga mkono*. 

Wasiliana na mkuu wa shule ya msingi uliyotoka au uliyosomea. Then kwa kila mtoto mmoja tu anayefanya vizur darasani unaweza kumfadhili kwa kumpa hata peni tu bure kwa mwaka mzima darasa la kwanza Hadi la Saba.  Pia Kama unauwezo ukaweza kuorganize  ukapata na wenzio watatu wawili hv mliofanikiwa kupitia elimu ya msingi pale. Mkafanya kwa ushirkiano as motivation and insperation kwa wadogo zenu. 


Baada ya kufanya hvyo. Naomba nitumie no. Ya mkuu wa shule na jina la shule uliyoanzisha program hiyo. Ili niweke kwenye kumbukumbu zangu. Mkoa, wilaya na kata ilipo. Hi itatudaidia kujua impact ya program yetu ktk shule hizo. 


*Ahnsanteni Sana karbuni Sana*.🤝


Imeandikwa na kuletwa kwenu na

*Eng. S. Ndaki*.


Phone: *0769866829* / *0684303536*

Email address: saimonndaki@gmail.com.

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU JINSI YA KUFANYA BIASHARA KIPINDI CHA MAGUFULI

CHALLENGE IS PART OF HUMAN LIFE