Habarin ya darasa la Sana na PhD.

 *❤️ANAANDIKA Eng. SAIMON.M.NDAKI❤️*

*Habari ya darasa la saba na PhD(Inauma)*

Kwa upendo mkubwa kabsa pia kupitia Imani na itikadi ya chama cha mapinduzi anayoiishi Eng. Ndaki ktk maisha yake ya kila siku.*Anaamini binadam wote ni sawa*

Kama mwana CCM Jasili, imala,hodari, makini na mtiifu aliyepikwa ndani ya itikadi ya CCM. Ameamua kusema kwa ufupi Sana kwa habari ya *Darasa la saba na PhD(Inauma)*.


Ndg. Zangu Watanzania wenzangu na wanachama wenzangu Jambo la Darasa la saba na PhD sio dogo na sio zuri kwa mahasrah mapana ya usitawi wa Taifa letu kwani linaumiza sana na kila kukicha limekuwa likichukua nafasi na kupamba Moto ndani ya jamii zetu, watoto, vijana, wazee na jamiii nzima.


Ndg. Zang wantanzania wenzangu Tukumbuke kwa miaka mingi Sana Taifa letu tumekuwa tukipambana kulitoa na kuling'atua na adui mkubwa kabsa wa Taifa letu *UJINGA* dira yetu ya pamoja ilikuwa ni kutokomeza kabsa adui UJINGA ktk Taifa letu kwani elimi ni ufunguo wa maisha. leo hii kumeibuka kasumba na tabia hatalishi na mbaya majukwaani, kwenye mitandao ya kijamiii na baadhi ya watu binafsi hususani wanasiasa kujitokeza na kusema *ELIMU SI CHOCHOTE SI LOLOTE*. 


Ndg. Zangu Watanzania Taifa hili bado changa na bado linahitaji wataramu na watoto wetu bado tunahitaji wasome ili kuepukana na janga hili la ujinga. Sasa tunakolipeleka tusipoangalia tunaliludisha tulikotoka miaka 50 ya Uhuru. Wahenga wanasema mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe na mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe. Sasa tusipokuwa makini tunaenda kuvunja nchi sisi wenyewe kupitia Hawa wenzetu wa *Darasa la saba na PhD(Inauma)* ni Kama utani vile Ila hatuwezi kuruhusu watu wataniane kwa niaba ya nchi yetu. 


Ndg. Zangu ni ukweli usiofichika kuna wenzetu ambao kupitia vitu vifuatavyo wanavitumia kupotosha jamiii. 

1. Uwezo wa kuongoza.

2. Ukosefu wa ajira.

3. Mfumo mbovu wa elimu yetu. 


 *(01) UWEZO WA KUONGOZA*


Ndg. Zangu Watanzania wenzangu Jambo la uwezo wa kuongoza watu au swala la uongozi Hilo anayetoa kipaji hicho ni MUNGU pekee lazima tulijue Hilo halihusiani kabisa na elimu ya hapa duniani. Uwezo wa akili ya mtu hiyo Mungu tu ndiyo anatoa. Sasa kumekuwa na kasumba ya watu kujinadi Mimi Darasa la ngapi, Mimi Prof, Mimi PhD, Mimi Eng. Ktk masuala ya  kuongoza watu. Jamani tubadilike tusichague viongozi kwa kuangalia elimu ya mtu. Kitu ambacho si sahihi hata ck moja. 


*(02): UKOSEFU WA AJIRA.*


Ndg. Zangu ni kweli Taifa letu lipo kwenye kipindi hicho wasomi wengi hawana ajira. Lazima Kama Taifa tupokee tatizo wote wasomi na wasio wasomi na baada ya hapo tutatue tatizo pamoja sio kuchekana na kubezana kana kwamba ukisoma ktk familia ni  dhambi Inauma Sana. *(Tuulizeni sisi tunaotoka kwenye familia za kifugaji shida tunayoipata ukisoma harafu ukose ajira)*.


*(03): MFUMO MBOVU WA ELIMU YETU.*


Ndg. Zangu Watanzania wenzangu ni ukweli usiofichika mfumo wetu wa elimu bado unahitaji malengo na mipango mipana ya kitaifa pamoja na kutoa UJINGA  lkn bado mfumo wetu hautusaidii vijana kuwa na tija ya kuendana na mabadiliko ya dunia inavyokwenda. 


🙏🙏🔥🔥🔥🔥🔥

Kwa hayo machache ndg. Zangu tizama Sasa watoto wetu wameanza kukimbia shule kwa hoja za wenzetu ambao wanapayuka payuka huko mtaaani kwamba *ELIMU SI CHOCHOTE SI LOLOTE* hata ukisoma ni kazi bure. Kitu ambacho ukikisikia kinaumiza Sanaaa. 😭😭. 


*Maswali ya kujiuliza*.👇👇👇👇👇👇👇👇


1. Tufanye nini ili Taifa letu liondokane na adui UJINGA? Maana hata Hawa wanaopayuka ovyo nao bado ni wajinga vilevile. 


2. Ni njia gani tutaitumia kutatua matatizo yetu Kama vile AJIRA na kuboresha mfumo wetu wa elimu. 


3. Tuko tayari kuliludisha Taifa hili kwenye Giza? 


4.  Tufanyeje? 

           Tufanyeje?

                Tufanyeje?❓

Nimeamua kuyasema haya Kama mzalendo wa Taifa langu na mtu ninayeumizwa Sanaaa, mnoooo na hali hii pale ninapoona ndg zangu, watoto wangu na rafiki zangu wameanza kukatatamaaa ya kusoma na kukimbia masomo haswa kwenye jamii zetu za WAFUGAJI. Ninaimani ndani ya group hili wapo watu wenye nafasi mbalimbali za kiutendaji watanisaidia kupaza sauti kwa jamiii zima na kufikisha ujumbe sehem husika especially *WABUNGE NA VIONGOZI MBALIMBALI MLIOPO HUMU* Natanguliza shukrani zangu kwenu. Ni ktk kujengana na kupanuana mawazo kwa mahasrahi mapana ya Taifa. Na palipo na shida, kukelwa na kuguswa. Bc ilikuwa ni mawazo yangu tu kwani nasitahili vitu viwili.

1.Msamaha nilipokosea. 

2. Pongezi  nilipopatia.


*Mungu awabariki Sana.*

*Mungu ibariki Tanzania*


Wenu ktk ujenzi wa Taifa

*Eng.SAIMON M. NDAKI(Mjumbe).*

mkutano mkuu mkoa wa CCM singida kutoka kata ya Muhalala. 


*Phone no*:0769866829/0684303536. 

*E-mail*: saimonndaki@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU JINSI YA KUFANYA BIASHARA KIPINDI CHA MAGUFULI

CHALLENGE IS PART OF HUMAN LIFE